Zimbabwe yapuuza miito ya walimwengu
18 Machi 2007Matangazo
Harare:
Wanaharakati wengine kadhaa wa upinzani wamekamatwa nchini Zimbabwe walipokua wakijaribu kusafiri.Msemaji wa chama cha Mageuzi ya kidemokrasi MDC,Nelson Chamisa amekamatwa na kupigwa vibaya sana hii leo alipokua uwanja wa ndege kuelekea Ubeligiji.Bwana Nelson Chamisa alikuwa aende Brussels kuhudhuria mkutano wa wabunge wa Umoja wa ulaya na nchi za Afrika,Caribian na Pacific.“Ameumizwa vibaya sana jicho na kichwa,amepoteza damu nyingi„ amesema msemaji wa kiongozi wa MDC,William Bango.Jana polisi wa Zimbabwe waliwazuwia wanaharakati wawili wa MDC,Sekai Holland na Grace Kwinje wasisafiri kwenda Afrika kusini kwa matibabu baada ya kupigwa vibaya sana pia mwishoni mwa wiki iliyopita.