1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mnangagwa atangaza uchaguzi Zimbabwe

18 Januari 2018

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amenukuliwa akisema taifa hilo litafanya uchaguzi katika kipindi cha miezi minne au mitano ijayo. Utakuwa uchaguzi wa kwanza kufanyika bila Robert Mugabe, tangu Zimbabwe ipate uhuru.

https://p.dw.com/p/2r6Do
Kombobild Mnangagwa (l) Mugabe (r)
Picha: AP

Zimbabwe itafanya uchaguzi katika muda wa miezi minne au mitano ijayo, gazeti moja limemnukuu rais Emmerson Mnangagwa akisema, ikiwa ndiyo mara ya kwanza tangu uhuru, kwa taifa hilo la kusini mwa Afrika litafanya uchaguzi ambao haumhusishi Robert Mugabe.

Kura hiyo, ambayo inatazamwa kama mtihani wa utambulisho wa demokrasia ya Mnangagwa, itakuwa muhimu katika kufungua milango ya msaada wa kifedha unaohitajika sana na taifa hilo, na kurekebisha uhusiano na mataifa ya magharibi na taasisi za kifedha za kimataifa.

Mnangagwa, mshirika wa karibu wa Mugabe, aliingia madarakani mwezi Novemba kufuatia uingiliaji kati wa kijeshi, wakati Mugabe mwenye umri wa miaka 93 alipolaazimishwa kujiuzulu baada ya jeshi kumzuwia katika jumba lake mjini Harare.

Simbabwe Emmerson Mnangagwa Rede in Harare
Rais Mnangagwa ameahidi uchaguzi wa kuaminika, haki na usio na mabishano, ili kuirejesha Zimbabwe kwenye nji ya demokrasia.Picha: Reuters/P. Bulawayo

Hii ndiyo lilikuwa hitimisho la mapambano ya kuwania madaraka kati ya Mnangagwa na mke wa Mugabe, Grace, ambaye alikuwa anaandaliwa na muwe wake kuchukuwa hatamu baada yake.

Shinikizo kwa Mnangagwa

Sasa Mnangagwa mwenye umri wa miaka 75, yuko chini ya shinikizo kutumiza ahadi yake ya kuboresha uchumi na kuonyesha kuwa anajitenga na sera ya Mugabe, ambaye utawala wake wa miaka 37 tangu uhuru mwaka 1980, ulibadili taifa hilo la matumaini na kuwa maskini na lililotengwa na mataifa ya magharibi.

Aliahidi kuwa uchaguzi wa urais, bunge na serikali za mitaa utakuwa wa amani na kuwaambia wafanyabiashara kuwa uwekezaji wao na faida vitakuwa salama.

"Zimbabwe inaeelekea katika uchaguzi katika muda wa miezi minne au mitano na tunapaswa kuhubiri amani, amani na amani kwa sababu tunajua ni nzuri kwetu na hatuna mashaka kwamba tutakuwa na uchaguzi wa amani," gazeti la serikali la Herald lilimnukuu Mnangagwa akisema wakati ziara rasmi nchini Msumbiji.

"Tutahakikisha kwamba Zimbabwe inaendesha uchaguzi huru, wa kuaminika, wa haki na usiobishaniwa, kuhakikisha kuwa Zimbabwe inashirikiana na dunia kama taifa lililofuzu kidemokrasia."

Wahlkampfveranstalatung der MDC in Simbabwe
Mpinzani mkuu wa Mnangagwa, Morgan Tsvangirai kutoka chama cha MDC hatarajii kuwania uchaguzi kutokana na kuugua maradhi ya saratani ya utumbo.Picha: AFP/Getty Images/Z. Auntony

Chini ya katiba, Zimbabwe inapaswa kuitisha uchaguzi kati ya Julai 22 na Agoti 22, lakini bunge linaweza kuchaguzua kujivunja, na hivyo kupelekea kufanyika kwa uchaguzi wa mapema. Chama tawala cha ZANU-PF kina wingi wa theluthi mbili katika bunge la sasa.

Tangu mwaka 2000, uchaguzi nchini Zimbabwe umekuwa ukikumbwa na vurugu za kisiasa na mabishano. Lakini kura ya mwaka huu wa 2018 inaweza kuukuta upinzani ukiwa haujajiandaa.

Mpinzani mkuu wa Mnangagwa Morgan Tvangirai anaugua maradhi ya saratani, ambayo yamesaidia kuweka wazi mipasuko ndani ya chama chake cha Movement for Democratic Change MDC, wakati ambapo maafisa wanagombaniwa uongozi wa chama hicho.

Mwandishi: Iddi Ssessanga/rtre

Mhariri: Daniel Gakuba