Zimbabwe yachaguliwa kuongoza halmashauri muhimu ya Umoja wa mataifa licha ya upinzani wa nchi za Magharibi na Marekani
12 Mei 2007Matangazo
Zimbabwe imekubaliwa kuongoza halmashauri muhimu ya Umoja wa mataifa yene jukumu la kusimamia maendeleo ya kiuchumi na ulinzi wa mazingira-licha ya upinzani wa Marekani ,nchi za Umoja wa ulaya na mashirika ya haki za binaadam.Halmashauri hiyo yenye wanachama 53 kuhusu maendeleo ya kudumu imeichagua Zimbabwe kwa kura 26 dhidi ya 21-tatu hazikuelemea upande wowote.Wadhifa wa mwenyekiti wa halmashauri hiyo ya nishati safi,hukabidhiwa kwa zamu mabara yote ya dunia-Mwaka huu ni zamu ya bara la Afrika.Katika duru ya mwisho ya majadiliano jana mjini New-York,Umoja wa Ulaya ulipinga kuidhinisha makubaliano yaliyofikiwa.Waziri wa mazingira wa serikali kuu ya Ujerumani Sigmar Gabriel-anaewakilisha pia Umoja wa ulaya amesema waraka wa mazungumzo hayo hauambatani na matarajio na unadhoofisha ahadi zilizochukuliwa mkutano kama huo ulipoitishwa miaka mitano iliyopita mjini Johannesburg