1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zimbabwe, ya kwanza kutumia chanjo ya India dhidi ya COVID

5 Machi 2021

Zimbabwe limekuwa taifa la kwanza barani Afrika kuidhinisha matumizi ya chanjo ya virusi vya corona iliyotengenezwa nchini India katika harakati zake za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/3qG0x
Bangladesch Sylhet | Corona | Start der landesweiten Impfkampagne
Picha: Md Rafayat Haque Khan/Zuma/picture alliance

Zimbabwe imeidhinisha matumizi ya chanjo ya virusi vya corona iliyotengenezwa na India na kuwa taifa la kwanza Afrika kuidhinisha matumizi yake kwenye kukabiliana na janga la Covid-19.

Hayo yametangazwa na ubalozi wa India nchini Zimbabwe muda mfupi baada ya mazungumzo kati ya balozi wa India na makamu wa rais ambaye pia ni waziri wa Afya wa Zimbabwe Constantino Chiwenga mjini Harare.

Katika mkanda mfupi wa video uliotolewa na wizara ya afya ya nchi hiyo Chiwenga amesema serikali ya India imetoa msaada wa dozi 75,000 za chanjo ya Covaxin na Zimbabwe inajitayarisha kununua chanjo zaidi kutoka India.

Chanjo hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Bharat Biotech, imeidhinishwa kwa matumizi nchini India ingawa takwimu za mafanikio yake kwenye hatua za mwisho za majaribio bado hazijatolewa.