Maoni mbele ya meza duara: Mada ni mvutano ndani ya chama tawala nchini Zimbabwe - ZANU-PF kuhusu atakayemrithi rais Robert Mugabe atakapoondoka madarakani pamoja na ushawishi wa mke wa kiongozi huyo Grace Mugabe. Mohammed Abdul-Rahman anawakaribisha Profesa Mwesiga Baregu kutoka Dar es Salaam, mchambuzi Martin Oloo kutoka Nairobi na mwandishi Nixon Katembo kutoka Johannesburg.