Zimbabwe katika Umoja wa Mataifa
17 Aprili 2008Kwa mara ya kwanza serikali ya Afrika kusini imeitisha kutangazwa haraka kwa matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Zimbabwe ambako kucheleweshwa sana matokeo kunaongiza hofu za kuzuka machafuko.
Katika Kikao cha Baraza la Usalama la UM mjini New York hapo jana,rais Thabo Mbeki wa Afrika kusini, akikwepa kulikabili swali la Zimbabwe ingawa ni yeye ndie aliepewa jukumu la kusuluhisha mzozo huo. Rama Yade,waziri mdogo wa mambo ya nje wa Ufaransa ,amesema Afrika kusini ni ufunguo wa ufumbuzi wa mgogoro wa uchaguzi wa Zimbabwe.
Mgogoro wa Zimbabwe jana ulihamia katika Baraza la Usalama la UM mjini New York,na ilitumainiwa kuupatia ufumbuzi,kwani wiki 3 sasa imeingia hakuna anaejulikana nani hasa ameshinda.
Rais Thabi Mbeki wa afrika kusini akihutubia kikao hicho makusudi akikwepa kuzungumzia mkasa wa Zimbabwe na hotuba yake ikijishughulisha zaidi na maswali jumla ya usalama na vipi kugharimia hatua za usalama huo barani Afrika.MMzozo wa zimbabwe hakuutaja hata kwa neno moja.Lakini hata kabla kuanza kwa kikao hicho, rais Mbeki akionekana ni ufunguo wa kitandawili cha Zimbabwe.
Bibi Rama Yade, waziri mdogo wa mambo ya nje wa Ufaransa anaehusika sana na maswali ya haki za binadamu akasema:
"Tunaiihitaji Afrika Kusini ikiwa tunataka ufumbuzi wa matatizo ya eneo hili."
Serikali ya afrika Kusini kwa mara ya kwanza leo imetoa sauti yake kudai matokeo ya uchaguzi wa urais wa Zimbabwe yatangazwe haraka.
Msemaji wa serikali Themba Maseko alisema mjini Cape Town na ninamnukulu,
"Hali ya mambo yatia wasi wasi."Akaongeza na ninamnukulu tena, " Uchaguzi unapofanywa na matokeo yake hayatangazwi wiki 2 baada ya uchaguzi huo,ni jambo la kutia wasi wasi mkubwa." mwisho wa kumnukulu. hili ni badiliko kubwa la serikali ya rais Thabo Mbeki aliedai hapo kabla utaratibu wa uchaguzi ufuate mkondo wake. Alidai pia kwamba hakuna mzozo wa uchaguzi wa Zimbabwe.
Msimamo huo wa rais Mbeki ukiangaliwa ni kumuungamkono rais Mugabe katika kuchelewesha matokeo.Isitoshe, serikali ya dola hili kubwa la kimkoa-Afrika Kusini, ikionekana hapo awali ikisitasita kujiunga na vilio vilivyopazwa ulimwenguni kupinga kucheleweshwa kutangazwa matokeo ya uchaguzi-uchaguzi ambao Upinzani unadai umeshinda. Hapo kabla, serikali ya Mugabe imemtuhumu Kiongozi wa chama hicho cha upinzani cha MDC,Morgan Tsvanigirai kufanya uhaini na kuwa inashirikiana eti na mtawala wa kikoloni Uingereza kumuangusha madarakani rais Mugabe.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alitaja athari kwa wakaazi wya Zimbabwe na hofu za kupotea imani katika mfumo wa kidemokrasia barani Afrika.
Katibu mkuu akapendekeza kupelekwa Zimbabwe kwa wachunguzi huru wa uchaguzi.
"Ushirikiano wetu katika mzozo wa Kenya ni mfano halisi unaoonesha jinsi tunavyoweza kufanikiwa endapo tukishirikiana pamoja."
Maneno makali na wazi yalisikika kutoka waziri mkuu wa uingereza Gordon Brown:
"Uchaguzi uliopitishiwa wizi wa kura sio uchaguzi wa kidemokrasi."
Nae mjumbe wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Khalidlzad aliwambia wajumbe kwamba mtu hawezi kuhudhuria kikao juu ya afrika bila kuzungumzia msukosuko wa sasa wa Zimbabwe."
►◄