1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zimbabwe imekua mwanachama wa kamisheni ya haki za binaadam ya umoja wa mataifa

28 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFIa

Zimbabwe imeteuliwa upya kua mwanachama wa kamisheni ya haki za binaadam ya umoja wa mataifa.Mataifa ya kiafrika katika umoja wa mataifa yameiteuwa Zimbabwe kua mojawapo ya wanachama wanne wa zoni ya Afrika katika taasisi hiyo yenye wanachama 15.Itakikalia kiti kwa kipuindi cha miaka mitatu ijayo.Marekani ambayo pia inawakilishwa katika kamisheni ya haki za binaadam ya umoija wa mataifa imeukosoa uamuzi huo.Mwanadiplomasia mmoja wa kimarekani anahoji uongozi wa Zimbabwe unakandamiza upande wa upinzani,unavunja uhuru wa vyombo vya habari, unawasumbua wanaharakati wa haki za binaadam na unawatia katika hali ya kuhofia usalama wao viongozi wa upande wa upinzani.