Zimbabwe hairuhusu wasimamizi wa kimataifa
6 Machi 2013Serikali ya Rais Robert Mugabe imesemakuwa haitaruhusu wasimamizi kutoka mataifa ya Magharibi kuja nchini Zimbabwe kusimia zoezi la utoaji maoni kuhusu katiba mpya ya nchi hiyo wiki ijayo. Sambamba na hayo pia iserikali hiyo imedai hakutakuwa na haja ya kuja wasimamizi hao katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika katikati ya mwaka huu.
Waziri wa mambo ya nje wa Zimbambwe Simbarashe Mumbengwi ameiambia DW kuwa Umoja wa Ulaya pamoja nchi nyingine za Magharibi hawataruhusiwa kuingia nchini Zimbabwe kwa ajili ya kusimamia utoaji wa maoni unatarajiwa kufanyika juma lijalo na kwenye uchaguzi utakaofanyika katikati ya mwaka huu. Amesama wasimamizi kutoka mataiafa ya Afrika tu ndio watakaoalikwa kusimamimi zoezi hilo la Maoni ya katiba na uchaguzi uajao.
''Ispokuwa zile nchi ambazo sio adui wa Zimbabwe zitakaribishwa hapa, ama nchi ambapo zimehusika katika kuiwekea Zimbabwe vikwazo vya aina yoyote ,hazitakuwa na ruhusa ya kuja kwenye uchaguzi na zoezi la kutoa maoni kuhusu katiba ya Zimbabwe'' amsema wazei wa mambo yanje wa Zimbabwe
Mapema mwaka 2002 nchi za Maghari ikiwemo Marekani na Umoja wa uala EU zilimuekea vikwazo vya kiuchumi Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe pamoja na ofisa mkuu wa chama chake cha Zanu P-F.
Uamuzi wa Mugabe wakosolewa
Vikwazo hivyo vilikuja baada ya kutolewa repoti ambayo ilikuwa inamtuhumu Mugabe kwa kukiuka haki za binadamu nchini Zimbabwe, ikiwemo wizi wa kura katika uchaguzi uliopita.
Kufatia taarifa hiyo balozi wa uingereza nchini Zimbabwe Deborah Borronert amesema kuwa ni vyema kwa serikali ya Mugabe kukaa na kupanga nani wa kumualika katika usimamizi huo wa maoni na uchuguzi ujao.Balozi Borronet akasema :-
'' Ni suala la kawaidi ulimwenguni kote kuwaalika wasimamizi wa uchuguzi wa kimataiafa, lakini bado itabaki kuwa ni chaguo huru kwa serikali yoyote inayofanya uchguzi kuamua nani wa kumaalika katika uchaguzi huo. Lakini nafikiria itakuwa jambo muhimu kwa serikali ya Zimbabwe kuwaalika wasimamizi wa kimataiafa katika zoezi hili.Umoja wa ulaya umekuwa na rekodi nzuri ya kutuma timu ya wasimamizi wa uchaguzi wenye mafunzo kuhusu kazi yao'' .
Donald Lewanika ambaye ni mkuu wa muungano wa kutatua migogoro na kushugulikia Demokrasia nchini Zimbabwe, ambaye pia amewahi kusimamia kesi ya uvunjaji wa haki za binadamu nchini humo ,ameikosao hatua hiyo ya serikali ya Mugabe na kusema kuwa ni hatua ya adhabu kwa wasimamizi hao wa maoni na uchaguzi.
Aliongeza kusema ,''Nafikiria jambo la msingi ambalo litaupa uchaguzi heshima, ni pale itakupokuwa uchaguzi umefanyika katika mazingira ya uhuru na uandilifu.Tunaposikia kwamba serikali inasema kuwa haitaruhusu wasimamizi kutoka nje, inatoa picha kwamba serikali inataka kuficha kitu katika zoezi hilo, ambacho haitaki wasimamizi hao kukiona''
Mwaka 2002 serikali ya Zimbabwe ilifuta viza ya kiongozi wa Umoja wa Ulaya ambaye alikuwa ni kiongozi wa timu hiyo ya wasiamamizi, hatua ambayo iliyafanya mataifa ya M agharibi kumuekea vikwazo Rais Robert Mugabe na wafuasi wake.
Mwandishi: Hashim Gulana
Mhariri:Moahammed Abdul-Rahman