1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya waziri mkuu wa Israel mjini Berlin

5 Desemba 2012

Tangazo la waziri mkuu wa Israel Netanyahu la kujenga makaazi 3000 ya kiyahudi katika ardhi za wapalastina,linatishia kugubika mazungumzo ya serikali za nchi hizi mbili mjini Berlin

https://p.dw.com/p/16wAi
Kansela Angela Merkel na waziri mkuu Benjamin Netanyahu wa IsraelPicha: dapd

Kimsingi ajenda ya mazungumzo ya siku mbili kati ya mawaziri wa seikali ya Israel na wenzao wa Ujerumani mjini Berlin ni ndefu:Mbali na mada za uhusiano na ushirikiano wa pande mbili mzungumzo hayo yatagubikwa pia na mzozo wa Mashariki ya kati na hali mpya iliyojitokeza hivi sasa.Hasa tangazo la waziri mkuu wa Israel la kujengwa majumba 3000 zaidi ya wahamiaji wa kiyahudi katika eneo la Jerusalem ya Mashariki na Ukingo wa magharibi wa Mto Jordan linatarajiwa kuzusha mabishano mazungumzoni.

Uhusiano mzuri pamoja na Israel ndio mhimili wa siasa ya nje ya Ujerumani.Jukumu la Ujerumani katika mauwaji ya halaiki ya wayahudi katika vita vikuu vya pili vya dunia limechangia katika hali hiyo.Katika miaka ya nyuma uhusiano huo daima umekuwa ukiimarishwa:Mawaziri wa serikali ya Ujerumani na Israel wanakutana kwa mara ya nne sasa tangu mwaka 2008.Ni lengo la Ujerumani kuchangia ili Israel,likiwa taifa la kidemokrasi na kiyahudi,iweze kuishi kwa amani na majirani zake."Amesema mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nchi za nje ya bunge la shirikisho Ruprecht Polenz .Lengo hilo linawezekana tu kuambatana na msingi wa ufumbuzi wa madola mawili-dola ya Israel na dola ya Palastina.Amesisitiza mwanasiasa huyo wa kutoka chama cha CDU.Ndio maana kansela Angela Merkel anabidi ashadidie upinzani wake dhidi ya mpango wa kujengwa makaazi 3000 mepya ya wahamiaji wa kiyahudi Mashariki ya Jerusalem na katika ukingo wa magharibi-kwasababu ujenzi huo ukavuruga uwezekano wa kufikiwa lengo hilo:amesisitiza bwana Ruprecht Polenz.

Siedlungsbau Israel
Makaazi ya wahamiaji wa kiyahudi katika ardhi ya wapalastinaPicha: Getty Images

Hata mwenyekiti wa kundi la wabunge wa kijerumani na kiyahudi,Jerzy Montag wa kutoka chama cha walinzi wa mazingira anataraji kansela Angela Merkel atazungumza kwa uwazi kabisa bila ya kuutia ufa msingi madhubuti wa uhusiano wa kihistoria wa nchi hizi mbili.

Katika mazungumzo kati ya mawaziri wa ulinzi,mambo ya nchi za nje na uchumi sawa na sekta nyengine,lawama hazitakosekana kutoka upande wa waisrael hasa baada ya Ujerumani kujizuwia kupiga kura hivi karibuni katika hadhara kuu ya Umoja wa mataifa badala ya kuyapinga moja kwa moja madai ya wapalastina ya kutambuliwa kama mwangalizi katika jumuia ahiyo ya kimataifa.

Deutsch-jüdisches Kulturerbe Gegenstand Israel
Ushahidi wa zana zinazotokana na urithi wa pamoja wa Utamaduni wa Israel na UjerumaniPicha: DW / Aya Bach

Licha ya hitilafu za maoni zilizoko,Berlin na Jerusalem zinashirikiana kwa dhati katika sekta ya usalama.Katika biashara ya silaha pamoja na nchi jirani ya kiarabu,mfano wa saud Arabia,kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje ya bunge la shirikisho Ruprecht Polenz anasema daima huzingatiwa masuala ya usalama wa Israel.Licha ya tofauti za maoni,Israel inajua inaweza kwa kila hali kuitegemea Ujerumani"Amemaliza kusema ruprecht Polenz.

Mandishi: Gorzewski,Andreas/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Mohammed Khelef