Ziara ya Bibi Clinton Nigeria
12 Agosti 2009Waziri wa nje wa Marekani bibi Hillary Cliinton, akiendelea na ziara yake ya nchi 7 za Afrika ilioanzia Kenya, ameendeleza leo kampeni yake ya kuhubiri utawala bora na demokrasia nchiniNigeria.Bibi Clinton , anatumai kuimarisha usuhuba na dola kuu hili lenye wakaazi wengii kabisa baranii Afrika na wakati huo huo, kupiga vtia rushua na mfarakano wa kidini nchini humo.Ajenda yake ya hii loe mjini Abuja, mji mkuu wa Nigeria, inajumuisha mazungumzo na Rais Umaru Musa Yar-Adua.
Mbali na mazungumzo yake hii leo na rais Yar-Adua, bibi Clinton akitarajiwa pia kuwa na mazungumzo ya meza ya duara na viongozi wa kidini nchinii Nigeriia.Hii inafuatia machafuko ya hivi karibuni na sehemu ya juhudi za Rais Obama kuunyoshea mkono wa suluhu na maskizano ulimwengu wa kiislamu.
Mshauri mkuu wa Bibi Clinton kwa maswali ya Afrika Johnnie Carson,waziri mdogo wa mambo ya nje kwa maswali ya Afriika,amesema uhusiano na Nigeria ni muhimu sana kwa usuhuba jumla wa Marekani na bara la Afrika.Hii inatokana na ukubwa wa Nigeriia na kwa visima vyake vya mafuta ambavyo viinalishiia mno mahitaji ya nishatii ya Marekani.
"Nigeria bila ya shaka ni nchi muhimu kabisa kusini mwa Jangwa la sahara." Carson aliwaambia maripota waliokuwamo ndani ya ndege ya Bibi Clinton iliokua ikielekea Abuja ikitokea Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo jana usiku.
Carson alisema zaidii kwamba, Marekani iimekuwa na uhusiano mwema na Nigeria mnamo miaka ya karibuni na ikapongeza mchango mkubwa wa Nigeria kimkoa pamoja na juhudi zake za kuituliza Sierra leone na Liberiia.Hatahivyo, alisema Carson, licha ya usuhuba huo mwema, Nigeria inakabiliwa na matatizo makubwa.
Alitaja hujuma zinazofanwa katika visima vyake vya mafuta katika Niger delta-hujuma ambazo zinaigharimu Nigeria mapipa alfu kadhaa ya mafuta kwa siku .Balaa jengine ni mripuko wa machafuko ya kidini ya madhehebu ya Boko haram katika miji kadhaa ya kaskazini mjwa Nigeria yaliosababisha vifo vya hadi watu 800-wengi wao waumiini wa madhehebu hiyo.
Utawala wa rais Barack Obama uliunyoshea mkono wa suluhu ulimwengu wa kiislamu ukitumai kupunguza sehemu ya hasira na uchungu miongonii mwa waislamu kutokana na sera za rais aliemtangulia (Obama)George Bush hasa juu ya vita nchini Iraq.
Afisa wa hadhi ya juu wa Marekani, akizungumza faraghani,amesema kwamba,Bibi Hillary Clinton, atawasikilza viongozi hao wa dini, lakini risala yake kuu itatuwama juu ya utawala bora na mageuzii juu ya mfumo wa uchaguzi. Rais Yar-Adua alishinda uchaguzi wa mwaka 2007 ambao wakaguzi walidaii ulipitishiwa mizengwe .
Katika ziara yake hiii nchini Nigeria, bibi Clinton atakuwa na jukwaa na waakilishi wa jami za kraia kuhusu njiia za kupambana na rushua nchinii Nigeria.Bibi Cliinton ameweka sharti la utawala bora kuwa ufunguo wa ziara yake hiii ya mataifa 7 ya Afrika iitakayomchukua piia Liberia na mwishoe ,visiwa vya Cape Verde.
Mwandishi:Ramadhan Ali/AFPE
Mhariri:M.Abdul-Rahman