Zelensky kuhutubia mkutano wa G7
6 Desemba 2023Zelensky atahudhuria sehemu ya kwanza ya mkutano huo utakaoongozwa na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida.
Ikiwa karibu miaka miwili baada ya uvamizi wa Urusi, dalili zinaongezeka kuwa uungaji mkono wa Ukraine kutoka kwa Magharibi unapungua wakati ambapo mapambano ya jeshi la Urusi yakionekana kuyumba, na wakati mapato ya mafuta ya Rais Vladmir Putin yakiimarika.
Soma zaidi: Zelensky kuwahutubia maseneta wa Marekani kufuatia msaada uliozuiliwa
Zelensky jana alifanya uamuzi wa ghafla wa kutohudhuria mkutano mwengine wa vidio hapo jana na maseneta wa Marekani.
Bunge la Marekani limegawanyika zaidi kuhusu uungaji mkono wa Ukraine kuliko ilivyokuwa wakati mwingine wowote katika vita hivyo, huku nchi hiyo ikionekana kuumaliza haraka msaada wa kujeshi uliotolewa na Marekani mpaka sasa.