Zelensky: Kipindi cha baridi Ulaya kitakuwa kigumu
4 Septemba 2022Kwa mara nyingine kinu cha nyukulia cha Zapozhizhya kimekuwa uwanja wa mapambano kusini mwa Ukraine licha ya uwepo wa ujumbe wa shirika la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyukilia IAEA. Shirika hilo limesema ugavi wa umeme ulikatwa. Voymbo vya habari vya Urusi viliripoti hapo awali kwamba njia za umeme ziliharibiwa kutokana na mapigano na kwamba ugavi wa umeme kwa ajili ya maeneo yanayodhitiwa na Ukraine ulikatizwa.
Hata hivyo Urusi imezungumzia juu ya vikwazo vilivyowekwa dhidi yake na nchi za maghgaribi kuwa ndio vilivyosababisha matatizo ya kiufundi na kutifua mvurugiko katika ugavi wa nishati.
Nchi za Ulaya zinazoiunga mkono Ukraine kijeshi na kidiploma zimeilaumu Urusi kwa kutumia nishati kama silaha ya kivita. Baadhi ya wachamabuzi wamesema kupanda kwa gharama za maisha wakati msimu wa baridi unakaribia kunaweza kudhoofisha msaada unaotolewa na nchi za magharibi kwa ajili ya serikali ya Ukraine.
Soma zaidi:IAEA kuweka ujumbe wa kudumu katika kinu cha Zaporizhzhia
Serikali za nchi za magharibi huenda zikalemewa na malalamiko ya wananchi wao. Wiki iliyopita Urusi ilisema italifunga bomba la kwanza la gesi lililoleta nishati hiyo nchini Ujerumani.
Nchi saba tajiri duniani za kundi la G7 zilitangaza kuweka kikomo katika bei ya mafuta kutoka Urusi. Urusi imesema haitauza mafuta kwa nchi yoyote inayotekeleza agizo hilo la nchi hizo saba tajiri. Kutokana na hali hiyo Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema Urusi si mshirika wa kuaminika tena.
Vyanzo: RTRE/DPA