1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky: Crimea lazima irudi mikononi mwa Ukraine

8 Aprili 2023

Rais wa Ukraine Volodomyr Zelensky amesema ni lazima nchi yake irejeshe udhibiti wa rasi ya Crimea iliyonyakuliwa kwa mabavu na Urusi mnamo mwaka 2014 na hakuna njia mbadala ya kupuuza dhamira hiyo.

https://p.dw.com/p/4PptG
Vifaa vya kijeshi vya Urusi
Vikosi vya Urusi ndani ya ardhi ya CrimeaPicha: Russian Defense Ministry/AP/picture alliance

Akizungumza katika hotuba ya kila siku kwa taifa Zelensky amesema heshima na nidhamu ya mahusiano ya kimataifa vitarejea duniani pale bendera ya Ukraine itakapopepea tena kwenye ardhi ya Crimea.

Kiongozi huyo alirejea matamshi hayo alipofanya mazungumzo na wanajeshi waislamu wa nchi yake ikiwemo wawakilishi wa jamii ya wachache wa Tatars ambao asili yao ni kutoka rasi ya Crimea.

Zelensky ametoa msimamo huo siku kadhaa baada ya rais wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva kupendekeza kuwa Ukraine iachane na mipango ya kuirejesha Crimea chini ya himaya yake kama sehemu ya mkataba wa amani kati yake ya Urusi