1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky atumia ziara yake Uingereza kuomba silaha

8 Februari 2023

Rais wa Ukraine Volodymy Zelensky ameitembelea Uingereza leo na kuomba msaada zaidi, ikiwa ni ziara yake ya pili ya kigeni tangu Urusi iliivamia Ukraine Februari 24 mwaka jana.

https://p.dw.com/p/4NFfY
England | Besuch Präsident Wolodymr Selenskyj | Treffen mit König Charles
Picha: Aaron Chown/Getty Images

Zelensky alifanya mazungumzo na Waziri Mkuu Rishi Sunak na kulihutubia bunge la Uingereza, ambapo alitoa wito wa kupelekwa ndege za kivita nchini Ukraine.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak aliliambia bunge kuwa Uingereza itaipa Ukraine msaada inaohitaji ili kuhakikisha inapata ushindi wa kijeshi kwenye uwanja wa mapambano mwaka huu.

Aidha amesema Uingereza itawapa marubani wa Ukraine mafunzo ya kuendesha ndege za kivita za viwango vya NATO.

Zelensky atafanya mkutano jioni hii na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Paris na kisha kesho Alhamisi mjini Brussels, ambako viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya wanakusanyika kwa mkutano wa kilele.