SiasaUkraine
Zelensky atia saini makubaliano ya kiusalama na Ubelgiji
28 Mei 2024Matangazo
Zelensky ametangaza makubaliano hayo ya dola bilioni 1.06 kupitia mtandao wake wa kijamii wa X.
Makubaliano hayo kando na mambo mengine yanaweka wazi ahadi ya Ubelgiji ya kuiunga mkono Ukraine katika muda wa miaka 10 ijayo.
Makubaliano hayo pia kwa mara ya kwanza yameeleza juu ya ndege 30 za kivita aina ya F-16 ambazo Ukraine itapokea, huku ndege ya kwanza ikitarajiwa kuwasili mwaka huu.
Makubaliano hayo ya usalama yametokea kufuatia uamuzi wa wakuu wa mataifa ya muungano wa NATO katika mkutano wa kilele uliofanyika mji mkuu wa Lithuania wa Vilnius mnamo mwezi Julai.
Wakati huo huo, mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kujaribu tena kuondoa kiunzi cha Hungary cha kuzuia mpango wa kuipa Ukraine msaada mpya wa fedha.