1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky ataka mahakama ya kuchunguza uhalifu Ukraine

4 Mei 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesisitiza kuwa ipo haja ya kuundwa mahakama maalumu ya kimataifa ya kuchunguza uhalifu uliofanywa na Urusi kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine

https://p.dw.com/p/4QuYC
Rais Volodomyr Zelensky wa Ukraine akiwa ziarani Uholanzi
Rais Volodomyr Zelensky wa Ukraine akiwa ziarani Uholanzi Picha: Robin van Lonkhuijsen/ANP/AFP via Getty Images

Akizungumza leo katika mahakama ya kimataifa ya Jinai iliyoko The Hague Uholanzi, Zelensky amesema Rais wa Urusi Vladmir Putin anastahili kuhukumiwa kwa vitendo vyake vya uhalifu.

Zelensky aliisifu kazi ya mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC iliyoanzisha uchunguzi dhidi ya vikosi vya Urusi kama vilifanya uhalifu wa kivita katika uvamizi wake Ukraine na pia kwa kutoa waranti wa kukamatwa kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin.