1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky ataka kuundwa mahakama kuchunguza uhalifu Ukraine

4 Mei 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesisitiza kuwa ipo haja ya kuundwa mahakama maalum ya kimataifa ya kuchunguza uhalifu uliofanywa na Urusi kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine

https://p.dw.com/p/4Qssu

Akizungumza muda mfupi uliopita katika mahakama ya kimataifa ya Jinai iliyoko The Hague Uholanzi, Zelensky amesema Rais wa Urusi Vladmir Putin anastahili kuhukumiwa kwa vitendo vyake vya uhalifu.

Mahakama ya ICC, ilianzisha uchunguzi kuhusu uwezekano wa uhalifu wa kivita uliofanywa na vikosi vya Urusi.

Mnamo mwezi Machi, mahakama hiyo ilitoa warranti wa kukamatwa kwa rais wa Urusi Vladimir Putin.

Ziara hiyo ya Zelensky ambayo haikutangazwa kabla, ndiyo ya kwanza kwake kufanya nchini humo.

Hadi sasa Uholanzi imeipa Ukraine msaada wa kijeshi unaokadiriwa kugharimu dola bilioni 1.32, kuisaidia nchi hiyo kujilinda dhidi ya uvamizi mkali wa Urusi.

Shirika la habari la Uholanzi limeripoti kuwa Zelensky atakutana pia na Waziri Mkuu wan chi hiyo Mark Rutte.