1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Askari wa Ukraine wakabiliana na vikosi vya Korea Kaskazini

6 Novemba 2024

Rais Volodymyr Zelensky amesema makabiliano ya kwanza kati ya jeshi la Ukraine na askari wa Korea Kaskazini yanafungua kile alichokiita ukurasa mpya wa kukosekana kwa utulivu duniani.

https://p.dw.com/p/4mhOW
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine
Rais Volodymyr Zelensky wa UkrainePicha: Remko de Waal /ANP/IMAGO

Hii ni baada ya waziri wake wa ulinzi Rustem Umerov kuthibitisha kuwa kulitokea mapigano madogo kati ya vikosi hivyo.

Zelensky amewapongeza viongozi wa ulimwengu waliojibu hatua ya kupelekwa vikosi vya Korea Kaskazini nchini Urusi mwezi uliopita sio tu kwa maneno, bali kwa kutayarisha hatua za kuunga mkono ulinzi wa Ukraine.

Soma pia:Zelensky adai wanajeshi 11,000 wa Korea Kaskazini wako Kursk

Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini imesema zaidi ya wanajeshi 10,000 wa Korea Kaskazini waliwasili Urusi huku idadi kubwa ya askari hao wakipelekwa kwenye viwanja vya mapambano, ikiwemo mkoa wa Kursk, ambako askari wa Ukraine walianzisha operesheni mwezi Agosti.

Wakati huo huo, Mawaziri wa mambo ya nje kutoka kundi la nchi saba tajiri duniani la G7 pamoja na nchi nyingine, wamelaani kuongezeka kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Korea Kaskazini na Urusi.