1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky apongeza hatua ya ndege za F-16 kupelekwa Ukraine

20 Agosti 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliye ziarani nchini Uholanzi ameupongeza uamuzi wa kuipa Ukraine ndege za kisasa za kivita chapa F-16 zinazonuiwa kuimarisha kikosi cha angani cha Ukraine.

https://p.dw.com/p/4VNTs
Wolodymyr Selenskyj trifft Mark Rutte in Eindhoven
Picha: ROB ENGELAAR/ANP/IMAGO

Tamko lake limejiri siku mbili baada ya Marekani kuidhinisha ndege hizo zilizopo Uholanzi na Denmark Kupelekwa Ukraine kujibu ombi la Kiev inayotaka silaha zaidi kutoka kwa washirika wake kujibu mashambulizi ya Urusi dhidi yake. 

Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte, amesema nchi yake iko tayari kupeleka ndege hizo pindi masharti yote ya kuwezesha hilo kufanyika yatakapotimizwa. Katika Mkutano wa pamoja na waandishi habari Zelensky alisema hatua iliyochukuliwa ni ya kihistoria, iliyo na nguvu na inayoleta matumaini.

Mafunzo ya matumizi ya ndege F-16 yaanza Ukraine

Awali Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksiy Reznikov alisema wanajeshi wa Ukraine wameanza kufunzwa namna ya kutumia ndege hizo na mafunzo hayo huenda yakachukua miezi sita au zaidi kukamilika. Ndege hizi zitaanza kusafirishwa baada ya mafunzo hayo kukamilika.