1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky anamshutumu Putin kwa uhalifu mpya wa kivita

23 Novemba 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemtuhumu Kiongozi wa Urusi Vladimir Putin kwa uhalifu mpya wa kivita kufuatia mashambulizi kwenye mji wa Dnipro, ambako urusi ilitumia kombora jipya la masafa ya kati.

https://p.dw.com/p/4nLWU
Der ukrainische Präsident Wolodymyr Selenskyj
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, katikati, anafahamishwa kuhusu hali ya mstari wa mbele na Brig. Jenerali Oleksandr Lutsenko, Novemba 18, 2024Picha: IMAGO/ZUMA Press Wire

Katika hotuba yake ya jana jioni kwa njia ya vidio Zelensky amesema mtu anapoanza kutumia nchi zingine sio tu kwa ugaidi, bali pia kwa majaribio yao makombora mapya kupitia ugaidi, hakika huo ni uhalifu wa kimataifa. Hapo awali, Putin alielezea matumizi ya kombora la masafa ya kati kama mtihani wa mafanikio chini ya hali ya vita. Serikali ya Kremlin inashutumu Kiev na Mataifa ya Magharibi kwa kuchochea vita na kusema matumizi yake ya kombora jipya ni jibu la kushambuliwa kwa eneo la Urusi na Ukraine kwa kutumia silaha za masafa marefu za Magharibi.