1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky ameonya kusambaratika ushirikiano wa Magharibi

7 Desemba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewaambia wakuu wa kundi la G7 Urusi imewaongezea shinikizo wanajeshi walio mstari wa mbele na kuonya juu ya hofu ya ushirikiano wa magharibi kusambaratika mwaka ujao.

https://p.dw.com/p/4ZrkG
Ukraine | Krieg | Frontbesuch Präsident Selenskyj
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy na kamanda wake wa vikosi vya ardhini Oleksandr Syrskyi.Picha: Ukrainian Presidency/ZUMA Wire/IMAGO

Mkutano huo kwa njia ya mtandao na ambao umehudhuriwa na washirika muhimu ambao ni pamoja na Ris Joe Biden wa Marekanina Rishi Sunak, Waziri Mkuu wa Uingereza, unafanyika wakati kuna mashaka ya mataifa hayo kupunguza misaada nchini Ukraine kutokana na mkwamo katika uwanja wa vita.Zelensky aidha ametoa wito kwa Umoja wa Ulaya kutimiza ahadi ya kuanzisha mazungumzo na Kyiv ya kujiunga na umoja huo, wakati wanachama wakijiandaa na mkutano wa kilele wiki ijayo.Kwenye taarifa yao, viongozi hao waG7 wamesema bado wana nia ya kuendelea kuisaidia Ukraine na kusaka njia bora zaidi za kuidhibiti Urusi kufadhili vita hivyo.