1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky akutana na waziri mkuu wa Ireland

13 Julai 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekutana na Waziri Mkuu wa Ireland Simons Harris hii leo katika uwanja wa ndege wa Shannon ulioko magharibi mwa Ireland

https://p.dw.com/p/4iFup
Flugabwehrsystem vom Typ Patriot | Ukraine-Konferenz - Mecklenburg-Vorpommern
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameizuru Ireland Picha: Jens Büttner/dpa/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekutana na Waziri Mkuu wa Ireland Simons Harris hii leo katika uwanja wa ndege wa Shannon ulioko magharibi mwa Ireland.

Mazungumzo hayo ni ya mara ya kwanza baina ya mataifa hayo mawili kufanyika huko Ireland na yamejikita zaidi kuviangazia vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine.

Soma zaidi. Zelensky kukutana na Waziri Mkuu wa Ireland

Zelensky alitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Shannon mchana wa leo akipokelewa na mwenyeji wake Simons Harris ambaye aliongozana na Balozi wa Ukraine nchini Ireland Larysa Gerasko.

Harris ametoa salamu zake za pole kwa raia ambao Ukraine imewapoteza kutokana na vita vinavyoendelea hususan shambulizi la hivi karibuni la kulipuliwa kwa hospitali kubwa ya watoto nchini Ukraine.

Na pia amemueleza Zelensky kuwa Ireland inaiunga mkono kikamilifu Ukraine katika juhudi zake kutaka kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.