1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zawadi nono kwa timu ya taifa ya Ujerumani

1 Aprili 2016

Wachezaji wa timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani – Die Mannschaft watapokea bahashishi ya euro 300,000 kila mchezaji ikiwa watashinda Kombe la Mataifa ya Ulaya . Euro 2016

https://p.dw.com/p/1IOFY
Fußball Länderspiel Deutschland - Italien
Picha: Reuters/M. Dalder

Shirikisho la kandanda la Ujerumani – DFB limesema licha ya kinyang'anyiro cha mwaka huu kuwa na timu nyingi na hatua nyingine ya mechi za mchujo, viwango vya bahashishi vitakuwa sawa na vya Euro 2012 ambapo Ujerumani iliondolewa katika nne za mwisho. Wachezaji watapokea euro 50,000 kwa kutinga robo fainali, 100,000 kwa kujikatia tikiti ya nusu fainali na 150,000 kwa kutinga fainali.

Ikiwa watashindwa katika htua ya 16 za mwisho, au washindwe kufuzu katika Kundi lao wataambulia patupu. Washindi hao wa Kombe la Dunia 2014, ni miongoni mwa timu 24 zinazopigiwa upatu kufanya vyema katika dimba hilo litakaloandaliwa Ufaransa kuanzia Juni 10. Wako katika Kundi C pamoja na Ukraine, Poland na Ireland ya Kaskazini. Meneja wa timu Oliver Bierhoff amesema baada ya makubaliano kati ya DFB na wachezaji kuwa “hilo litaleta amani na uwazi kabla ya dimba hilo kuanza“

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Khelef