Zanzibar kutumia shilingi bilioni 7.5 kwa uchaguzi
13 Oktoba 2015ZEC inasema imejipanga kuwaita wadau wa uchaguzi kuwaeleza ukamilishaji wa taratibu za uchaguzi ambazo zinakaribia kufikia ukingoni mnamo tarehe 25 Oktoba, huku masuali kadhaa ya khofu na kasoro za uchaguzi huo yakiibuka kutoka kwa wanasiasa kuhusiana na matayarisho hayo.
Katika kikao cha pamoja cha maandalizi ya uchaguzi kati ya ZEC na wadau wa vyama vya siasa, Mwenyekiti wa Tume hiyo Jecha Salum amesema serikali imetenga jumla ya shilingi billioni 7. 5 kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar na tayari tume imeshaingiziwa shilingi billioni 2.5 hadi sasa.
Mwenyekiti huyo alisema katika kuhakikisha wamejipanga vyema wametenga kituo maalumu cha kutangazia matokeo ya uchaguzi, na Makamo wake, Abdulhakeem Ameir Issa, amelitaja eneo hilo kuwa ni hoteli ya Bwawani.
Sikiliza mahojiano kati ya Salma Said na Mkurugenzi wa ZEC, Salim Kassim.