1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zanzibar. Clinton awataka viongozi wa zanzibar kuwataka wananchi kutowanyanyapaa wagonjwa wa ukimwi.

22 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEs3

Rais wa zamani wa Marekani Bwana Bill Clinton jana amewataka viongozi wa Zanzibar nchini Tanzania kupambana na hali ya kujihisi aibu na kuwanyanyapaa wagonjwa wa ukimwi ili kuweza kuimarisha juhudi za kuzuwia kuenea kwa ugonjwa huo hatari.

Wakati mataifa mengine yamepiga hatua , wagonjwa kiasi ya 6,000 wa ukimwi katika eneo hilo lenye utawala wake wa ndani katika muungano wa Tanzania , mara kwa mara hujikuta wakiathirika kutokana na hisia za fedheha, maafisa wamesema.

Zanzibar ina wakaazi karibu milioni moja, ikiwa asilimia 98 ni Waislamu.

Bwana Clinton amesema kuwa ujumbe anaotoa ni kuwa viongozi wahakikishe , hakuna uwanyanyapaa dhidi ya wagonjwa wanaoishi na virusi vya ukimwi. Ameyasema hayo baada ya kuwatembelea wagonjwa katika hospitali kuu ya Mnazi mmoja mjini zanzibar jana.