ZANU PF yadai kura zihesabiwe upya
6 Aprili 2008Harare:
Chama cha ZANU-PF cha rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kimelikataa shauri la upande wa upinzani la kushiriki katika serikali ya umoja wa taifa,na kutoa mwito kura za uchaguzi wa rais wa March 29 iliyopita zihesabiwe upya.Licha ya kushindwa katika uchaguzi wa bunge,chama tawala cha ZANU PF, kupitia jarida la Sunday Mail,kinaonyesha ukakamavu.Waziri wa sheria Patrick Chinamasa amenukuliwa na Sunday Mail akisema hawawezi kushirikiana na MDC kwasababu malengo yao ya kisiasa na matarajio yao ni tofauti sawa na ardhi na mbingu."Mwisho wa kumnukuu bwana Chinamasa.ZANU PF kimeitaka kamisheni ya uchaguzi ihesabu upya kura ,kikihoji pamefanyika makosa katika zowezi la kuhesabiwa kura.Wakati huo huo kamisheni ya uchaguzi imetangaza matokeo ya uchaguzi wa baraza la Senet ambapo vvyama vyote viwili,ZANU-PF na MDC kinachoongozwa na Morgen Tsvangirai vimejinyakulia kila mmoja viti 30 kati ya 60 vya baraza hilo la Senet.Na korti moja ya mjini Harare inatazamiwa kutathmini hii leo madai ya chama cha upinzani cha MDC kutaka matokeo ya uchaguzi wa rais yatangazwe haraka.