1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZANU PF na MDC kuanza mjadala kuhusu mkwamo wa kisiasa

Kalyango Siraj21 Julai 2008

Je! Muafaka kupatikana kuanzia leo?

https://p.dw.com/p/Eg98
Morgen Tsvangirai ,kushoto, na Robert Mugabe,kulia.Picha: AP

Vyama viwili vikuu vya kisiasa nchini Zimbabwe,chama tawala cha ZANU PF na kile cha upinzani cha MDC vinatarajiwa kutia saini mkataba wa kukubaliana kuanza mazungumzo kamili kuhusu mgogoro wa kisiasa unaoikumba nchi hiyo japo chama cha upinzani kinaweka msharti.

Hii inafutaia juhudi mbalimbali za kutaka pand hizo mbili kuzungumza.

Taarifa kutoka Zimbabwe,zikimnukuu afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa, zinasema kuwa chama cha rais Mugabe cha ZANU PF pamoja na cha mpinzani wake mkuu kisiasa Morgen Tsvangirai cha MDC, kimsingi, vimekubaliana kuhusu mazungumzo yenye nia ya kumaliza mgogoro wa kisiasa.

Makubaliano hayo ni kuhusu kuanza mazungumzo rasmi.Taarifa zilizotolewa awali zilionyesha kama hati ya kukubali kuanza mazungumzo hayo yaweza ikatiwa saini leo jumatatu.

Lakini chama cha upinzani kilisema kuwa hakitatia saini makubaliano hayo hadi mpatanishi Afrika Kusini atakapo shughulikia manunguniko yao.

Hapo awali mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Zimbabwe,Haile Menkerios,alinukuliwa kusema kuwa,kama hatua ya kwanza kuelekea hilo, muswada jaribio umeshakubaliwa na pande zote mbili yaani rais Mugabe na Bw Tsvangirai.

Ingawa pande husika katika mazungumzo zimeonyesha matarajio yao ya makubaliano hayo kutiwa saini leo,lakini msemaji wa Bw Tsvangirai pamoja na cheo somo wake wa mpatanishi wa mzozo huo rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki hawakutoa hakikisho la kutokea hilo.

Hata hivyo taarifa za hivi punde kutoka Zimbabwe zinasema kuwa pande hizo mbili zitatia saini makubaliano hayo hii leo mchana saa za Zimbabwe.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, waziri wa Sheria wa Zimbabwe,ambae pia ndie kiongozi wa ujumbe wa chama cha rais Mugabe katika mazungumzo hayo,Patrick Chimasa,makubaliano yatatiwa saini leo jumatatu.

Makubaliano ya leo jumatatu,ikiwa yatafikiwa ni ya kukubaliana kuanza rasmi mazungumzo ili kutafuta muafaka wa mgogoro ambao umekuwa ukiendelea kwa mda sasa.

Shinikizo limekuwa likiongezeka la kutaka kufikia muafaka kuhusu uchaguzi tatanishi wa Juni 27 ambao ulimpatia ushindi rais Mugabe bila ya kushiriki kwa mpinzani wake Tsvangirai ambae alijiondoa akidai wapinzani wake walikuwa wakinyanyaswa.

Chama cha MDC kimekataa kumtambua Mugabe kama mshindi wa uchaguzi huo,kikishikilia msimamo wa kuwa, kiongozi wao Tsvangirai alishinda duru ya kwanza ya ucnaguzi uliofanyika machi.Hata hivyo takwim rasmi zilionyesha kama hakupata idadi ya kumpa ushindi wa moja kwa moja na hivyo ikabidi kufanyika kwa duru ya pili.

Wasiwasi ulijitokeza baada ya kura hiyo ya marudio, na umevuruga zaidi uchumi wa nchi hiyo ambapo mfumuko wa bei umepanda kupita asili mia millioni 2,kusababisha uhaba wa mahitaji muhimu mkiwemo chakula na pia ukosefu wa ajira kupanda kwa asili mia 80.