Zaidi ya watu milioni nne wameyakimbia makazi yao Ethiopia
24 Agosti 2023Matangazo
Ripoti ya Shirika la Wahamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM, kuhusiana na watu wanaoyakimbia makaazi yao nchini humo imesema jumla ya watu milioni 4.38 wameyakimbia makaazi yao kuanzia Disemba 2022 hadi Juni 2023.
Kulingana na ripoti hiyo iliyochapishwa jana Jumatano, mizozo iliongoza kwa kuchochea tatizo hilo kwa asilimia 66.41 na ukame ukichangia kwa asilimia 18.49.
Zaidi ya watu milioni moja waliukimbia mkoa wa Tigray uliokumbwa na machafuko.
Jumla ya watu milioni 28 nchini Ethiopia wanahitaji msaada, hii ikiwa ni kulingana na takwimu za umoja huo.