1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu bilioni 1 duniani ni wanene kupindukia

1 Machi 2024

Utafiti uliotolewa na jarida la matibabu la Lancet unaonesha kwamba zaidi ya watu bilioni moja duniani kwa sasa wanakabiliwa na unene kupita kiasi.

https://p.dw.com/p/4d3df
Unene wa kupindukia
Watu wenye unene wa kupindukia wazidi kuongezeka duniani.Picha: Dominic Lipinski/empics picture alliance

Jarida hilo linasema idadi hiyo imeongezeka zaidi ya mara nne tangu mwaka 1990.

Utafiti huo uliofanywa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) unaonesha kwamba "janga" hilo hasa linazikumba nchi maskini duniani na idadi inaongezeka kwa haraka zaidi miongoni mwa watoto na mabaleghe kuliko kwa watu wazima.

Soma zaidi: Ripoti: Dunia itakuwa na watu wanene kupita kiasi 2035

Utafiti huo uliotolewa kuelekea maadhimisho ya Siku ya Unene wa Kupitiliza mnamo Machi 4, unakadiria kwamba kulikuwa na karibu watu wazima, mabaleghe na watoto milioni 226 waliokuwa na unene wa kupita kiasi mwaka 1990.

Kufikia mwaka 2022, idadi hiyo ilikuwa imeongezeka na kufikia watu bilioni moja milioni 38.

Mkurugenzi wa lishe kwa ajili ya afya katika shirika la WHO, Francesco Branca, amesema ongezeko hilo la kuvuuka bilioni moja limetokea mapema zaidi kuliko makadirio waliyokuwa nayo.