Watu 60 wahofiwa kufa katika vita kati ya makundi ya jihadi
21 Novemba 2023Matangazo
Vyanzo vimeliambia shirika la habari la AFP kuwa, mapigano yalianza kuanzia Ijumaa hadi Jumamosi baada ya wapiganaji wa ISWAP walipovamia boti za Boko Haram katika ziwa Chad linaloizunguka Nigeria, Niger, Cameroon na Chad.
Vyanzo hivyo vimeeleza kuwa waliokuwemo ndani ya boti hizo wakiwemo wavuvi na wanawake wa jamii ya Fulani waliokuwa wametekwa nyara na Boko Haram.
Makundi hayo mawili ya jihadi yameingia katika vita vikali vya kuwania mamlaka, huku kukiwa na mapigano makali kati yao tangu kundi la ISWAP lilipojitenga mwaka 2016.
Mapigano hayo yaliongezeka kufuatia kifo cha kiongozi wa Boko Haram mwaka 2021 wakati wa mapigano katika ngome ya msitu wa Sambisa.