1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya watu 20 wauwawa Ethiopia

24 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/E5KV

Zaidi ya watu 20 wameuwawa katika siku tatu za mapigano yaliyochochewa na suala la ardhi huko magharibi mwa Ethiopia.Polisi nchini humo imefahamisha hii leo kwamba vita hivyo vimekuwa vikiendelea katika maeneo ya mpaka kati ya jimbo la Oromia na Benishangule.Hata hivyo polisi imekanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba mapigano hayo yamesababisha kuuwawa watu zaidi ya 100. Mapigano katika eneo hilo yanayotokana na mivutano kuhusu maeneo ya malisho ya mifugo na ardhi ya mashamba yamekuwa yakishuhudiwa mara kwa mara,mwezi Aprili vita juu ya suala la ardhi kusini mwa Ethiopia katika mji wa Wondo-Genet yalisababisha mauaji ya watu 18.