1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaCameroon

Zaidi ya wanawake 30 wametekwa nyara Cameroon

24 Mei 2023

Wanawake 30 wametekwa nyara Cameroon na wanamgambo wanaopigania kujitenga

https://p.dw.com/p/4Rjw2
Symbolbild I Cameroon anglophone rebel
Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Maafisa wa serikali wamesema utekaji nyara huo ulitokana na wanawake hao kupinga ushuru haramu wanaotozwa na wanaharakati hao.

Afisa wa ngazi ya juu katika eneo hilo amesema wanawake hao walichukuliwa katika kijiji cha Babanki, karibu na mpaka na Nigeria.

Afisa huyo kwa jina Emil Mooh ameongeza kuwa wengi wa wanawake hao waliteswa na bunduki na mapanga.

Mooh amesema wapiganaji hao walikuwa wanakusanya malipo ya kila mwezi kutoka kwa watoto, wanawake na wanaume.

Wanawatoza wanandoa ushuru kabla ya kuoana, na kuzilazimisha familia kulipa dola 1,000 ili kuwazika jamaa zao.

Cameroon imekumbwa na mapigano tangu wanaharakati wa eneo kunakozungumzwa Kiingereza walianzisha uasi mwaka wa 2017.

Waasi hao wametangaza lengo la kujitenga na eneo lenye wakaazi wengi wanaozungumza Kifaransa na kutengeneza mkoa huru, wa wanaozungumza Kiingereza.