1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya wakimbizi 50 wauawa Ituri, Congo

2 Februari 2022

Wakimbizi zaidi ya 50 wameuawa usiku wakuamkia leo Jumatano katika kijiji cha Ngujona wilayani Djugu katika mkoa wa Ituri. Yamefanyika wakati juhudi zinaendelea za kuwahamasisha waasi kuzisalimisha silaha zao

https://p.dw.com/p/46P5W
DR Kongo | Nord Ost Ituri | Menschenrechtsverletzungen
Picha: Tom Peyre-Costa/NRC

Akizungumza na DW kwa njia ya simu, kiongozi wa utawala wa Bahema Badjere Jean-Richard Dedha alisema, kuwa waasi wa CODECO walijipenyeza kwenye kambi ya wakimbizi Savo katika kijiji cha Ngujona,saa nne za usiku na kuwauwa wakimbizi pamoja na kuwakeruhi wengine wengi. 

Chifu Jean-Richard Dedha anatuambia jinsi walivyouawa wakimbizi hao zaidi ya hamsini, pale akitupatia hali inayojiri katika kijiji cha Ngujona, baada ya shambulizi hilo ( O-ton Chifu)

Mauwaji haya kwa mara nyingine yanafanyika, wakati mikoa ya Kivu ya Kaskazini pamoja na Ituri ikiwa katika hali ya dharura, viongozi wa jeshi wakiwa waliteuliwa na rais Félix Tshisekedi, ili kukabiliana ipaswavyo na makundi ya waasi katika mikoa husika. 

DR Kongo | Nord Ost Ituri | Menschenrechtsverletzungen
Makundi ya waasi yanatatiza mashariki mwa CongoPicha: Tom Peyre-Costa/NRC

Kusuasua kwa operesheni za kuwatokomeza waasi katika mkoa wa Ituri pamoja na mauwaji ya kila mara, John Kabwa mmoja wa wazee wa busara wa kabila la Bahema, pamoja na kulaumu mauwaji ya wakimbizi, anatoa mwito huu kwa rais Félix Tshisekedi 

Aidha waasi wa CODECO wanawauwa wakimbizi, wakati pametumwa Bunia tume ya viongozi wa zamani wa makundi ya waasi, ilikuwahamasisha wapiganaji wa makundi ya waasi kuzisalimisha silaha zao. Wajumbe wa timu hiyo inayoongozwa na Thomas Lubanga kiongozi wa kundi la zamani la uasi UPC,wamekuwa wakikutana kwa mazungumzo na wajumbe wa makabila mbalimbali ya Ituri pamoja na mashirika mbalimbali ili kuwahamasisha kuhusu amani.

Na huko hayo yakiwa namna hiyo, askari wa jeshi la Uganda UPDF wamepelekwa katika wilaya ya Irumu mkoani Ituri, kukabiliana na waasi kutoka Uganda ADF, wanaowauwa wakaazi katika wilaya hiyo,kuteketeza vijiji, kuchoma moto magari pamoja na pikipiki.

Kutumwa huko kwa wanajeshi hao wa UPDF katika operesheni za pamoja na jeshi la Congo FARDC, kunadhaniwa na wengi kwamba kutachangia pakubwa katika kuwatokomeza waasi katika wilaya hiyo. 

John Kanyunyu - DW Beni