1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MafunzoBurkina Faso

Zaidi ya shule 5,700 zimefungwa nchini Burkina Faso

24 Novemba 2022

Zaidi ya shule 5,700 zimefungwa nchini Burkina Faso kutokana na hali ya usalama, huku wanafunzi milioni moja wakinyimwa fursa ya kusoma. Haya ni kwa mujibu wa shirika la msaada la Save the Children.

https://p.dw.com/p/4JzQb
Architektur l Francis Kere, Grundschule in Gando
Picha: Nicolas Remene/Le Pictorium/MAXPPP/dpa/picture alliance

Katika taarifa,  shirika hilo limesema kwamba Idadi hiyo mpya ni maradufu ya ile iliyotangazwa na serikali mapema mwaka huu.

Wanajeshi wa Burkina Faso Na Mali wakutana kujadili usalama

Tangu mwaka wa 2017, makundi yenye silaha ya Kiislamu yamekuwa yakilenga walimu na shule nchini Burkina Faso, na kutangaza upinzani wao dhidi ya elimu ya nchi za Magharibi na taasisi za serikali.

Kulingana na wizara ya elimu, zaidi ya walimu 28,000 wameathiriwa na kufungwa kwa shule hizo.