Zaidi ya maafisa 1,000 wajeruhiwa katika maandamano Ufaransa
2 Aprili 2023Ufaransa imekumbwa na migomo na maandamano baada ya Rais Emmanuel Macron na serikali walipitisha mipango ya kuongeza umri wa kustaafu hadi 64 kutoka 62.
Soma pia: Maandamano yaendelea Ufaransa kupinga mageuzi ya pensheni
Darmanin ameliambia gazeti la Ufaransa la Journal du Dimanche kuwa kulikuwa na matukio 2,579 ya moto na mashambulizi 316 kwenye majengo ya umma tangu maandamano hayo yalipoanza mwezi Machi.
Hakutoa idadi ya waandamanaji waliojeruhiwa, lakini alisema maafisa 36 wanachunguzwa kwa tuhuma za matumizi ya nguvu kupita kiasi. Darmanin amepinga tuhuma kuwa polisi waliwashambulia waandamanaji na kutumia nguvu kupindukia.
Alisema polisi walihitajika kuingilia kati wakati maandamano hayo ya amani yaligeuka kuwa vurugu. Vyama vya wafanyakazi vimetangaza siku ya 10 ya migomo na maandamano ya kitaifa Alhamisi wiki ijayo, huku serikali ikionyesha dalili za kutosalimu amri kuhusu mageuzi hayo mapya.