1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBangladesh

Yunus asifu ´ukombozi wa pili´ wa Bangladesh

8 Agosti 2024

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Muhammad Yunus amepongeza kile alichokiita "ukombozi wa pili" wa Bangladesh.

https://p.dw.com/p/4jGE6
Bangladesh Dhaka | Muhammad Yunus
Muhammad Yunus baada ya kula kiapo kuongoza serikali ya mpito ya Bangladesh.Picha: MUNIR UZ ZAMAN/AFP

Ameyasema hayo baada ya kurejea kuirejesha nchi yake katika mkondo wa demokrasia baada ya maandamano yaliyoongozwa na wanafunzi kuuhitimisha utawala wa miaka 15 wa Waziri Mkuu Sheikh Hasina.

"Bangladesh ni familia. Tunapaswa kuiunganisha. Tunataka kuondoa shida yoyote iliyopo. Nataka kuwaleta wale waliopotea njia. Ili tufanye kazi pamoja." amesema Yunus.

Yunus mwenye umri wa miaka 84 ataongoza serikali ya mpito ambayo inaundwa na jeshi, ambalo lilimpa ngongo Hasina mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya mamia ya watu kuuawa katika maandamano yenye vurugu.

Akizungumza baada ya kuwasili mapema leo akitokea Ulaya, Yunus alitoa wito wa kurejeshwa utulivu baada ya vurugu zilizosababisha vifo vya watu 455.