1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DW lamkabidhi Nalvanaya tuzo ya uhuru wa kujieleza ya 2024

6 Juni 2024

Shirika la utangazaji la DW limemkabidhi Yulia Navalnaya pamoja na Wakfu wa Kupambana na Rushwa ya nchini Urusi Tuzo ya Uhuru wa Kujieleza kwa mwaka huu 2024.

https://p.dw.com/p/4ghtl
Tuzo ya Deutsche Welle ya Uhuru wa Habari ya Yulia Navalnaya
Tuzo ya Habari ya Shirika la DW la Ujerumani ambayo imemkabidhi Yulia Nalvanaya, mke wa aliyekuwa mpinzani mkubwa wa Putin, Alexei NavalnyPicha: DW

Hafla hiyo ilifanyika mjini Berlin jana Jumatano, ambapo Navalnaya aliwaambia waliohudhuria kwamba uhuru wa kujieleza ulikuwa silaha muhimu zaidi kwake na mumewe Navalny, katika kipindi cha miaka 13 walipokuwa wakijaribu kumpinga Rais Vladimir Putin.

Uamuzi wa kumtunuku Nalvanaya na FBK tuzo hiyo ulitangazwa mwezi uliopita.

Mkurugenzi Mkuu wa DW Peter Limbourg pamoja na Waziri wa Fedha wa Ujerumani Christian Lindner walimpongeza Navalnaya na marehemu mumewe, na Ivan Zhdanov wa FBK, ambaye ni mwanasheria na rafiki wa muda mrefu wa Navalny.

Wamesema tuzo hiyo inachukuliwa kama ukumbusho wa maana ya demokrasia na utawala wa sheria.