YEHUUU! Tumerudi tena na Karandinga
Awamu ya Tatu ya Karandinga
Mambo si ndiyo haya!
Watayarishaji na waandaaji wa vipindi vya Noa Bongo-Jenga Maisha Yako, wakiwa na baadhi ya waigizaji wa mchezo ya Karandinga inayozungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana barani Afrika.
Wahusika
Michezo yote ya Karandinga inaandikwa na watunzi wa Kiafrika. Hadithi zao zinaandaliwa vizuri sana hali inayomfanya muigizaji ajitambue hasa namna anavyopaswa kuigiza.
Tabasamu kazini
Kwa kawaida waigizaji huwa wanabadilishana mawazo wakati wa maandalizi ya kurekodi, lakini kikubwa kinachotuletea furaha zaidi ndani ya studio, ni pamoja na utani wa hapa na pale kiasi kwamba muigizaji hujisikia mwenye furaha muda wote na kumuacha na tabasamu kila dakika.
Sehemu muhimu
Waigizaji wakiwa katika mawazo mazito kutokana na aina ya hadithi wanayorekodi, hasa zikiwa zile zinazohusu masuala ya kisiasa, rushwa na uharibifu wa mazingira. Lakini kumbuka, waigizaji wa Karandinga wengi wamebobea katika tasnia ya uigizaji.
Kuileta hadithi katika uhalisia
Hapa kuna mama, mwalimu na mpelelezi. Mbali na tabasamu unaloliona, waigizaji hawa walifanikiwa vizuri katika kujiingiza kwenye uhalisia wa hadithi yenyewe. Kumbuka, uigizaji ni kipaji.
Maandalizi
Wakiwa studio, waigizaji wanafanya mazoezi kabla ya kuanza kurekodi. Hali hii husaidia sana kuwafanya wajiamini na waigize uhusika wao kikamilifu.
Vijana wanaopambana na taarifa za uwongo
Wahusika wakuu wa hadithi kuhusu taarifa za uongo kwenye mitandao ambao umepewa jina, ''Taarifa Nyingi, Moja ya Kweli.'' Mzome Mahmoud (Kushoto) aliyeigiza kama Fidelis, Rachel Kubo (Kati) aliyeigiza kama Kayla na Aloyce Michael (kulia) aliyeigiza kama Jammo. Vijana machachari kabisa!
Ni faraja kutembelewa na wageni
Tukiwa studio huwa tunatembelewa na wageni wa aina mbalimbali, kuanzia viongozi wa serikali hadi maafisa ubalozi. Pichani ni baadhi ya wageni waliotutembelea studio, akiwemo Andrea Schmidt, (wa pili kulia) ambaye ni Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili DW.