Yasiyo sahaulika katika ufunguzi wa mashindano ya Olimpiki
Bendelea ya Olimpik inaashiria amani baada ya Vita Vya I Dunia, wakati mwenge wa Heroshima ulipowashwa mjini Tokyo 1964. Hafla ya ufunguzi imejikita zaidi katika historia ya kisisa na mwamko zaidi.
1986: Michezo ya kwanza ya mchuano wa Olimpiki
Micheo ya Olimpiki ilikuwa maarufu Ugiriki katika kipindi cha miaka zaidi ya 1000 hadi ilipopigwa marufuku na Mfalme Theodosius kwa madai kuwa ulikuwa utaratibu wa kipagani. Msomi wa Kifaransa Pierre de Coubertin alinazisha mwamko mpya mjini Athens kuanzia April 5-15,1896, ambapo michezo hiyo ilifunguliwa na Mfalme George wa Ugiriki.
1920: Bendera ya kwanza ya Olimpiki na kiapo Antwerp
Si zaidi ya miaka miwili baada ya Vita Vya Kwanza vya Dunia miashindano ya Olimpiki yalifanyika Antwerp. Bendera ya Olimpiki ilipepea kwa mara ya kwanza ikiashiria amani duniani. Kiapo cha michezo ya Olimpiki kilitambulishwa katika kufanikisha ushindani wa haki wa michezo.
1928: Ugiriki ilianzisha utaratibu wa ishara Amsterdam
Mwaka 1928 katika michezo ya msimu wa kiangazi mjini Amsterdam, sehemu kubwa ya utaratibu wa sasa ulianzishwa. Ilikuwa mara ya kwanza kwa timu ya taifa ya Ugiriki kuingia uwanjani wakati wa gwaride la wanamichezo. Wachezaji kutoka nchi husika walishiriki kwa kuzingatia helufi kwa mujibu wa lugha iliyochaguliwa na nchi husika.
1936: Manazi wa Ujerumani walianzisha mbio za Mwenge
Manazi walikuwa hodari kwa kutumia ishara-na walianzisha nembo kadhaa ambazo zinashuhudiwa mpaka leo hii. Kwa mara ya kwanza, mwenge wa Olimpiki ulitembezwa kutoka Athens mpaka Berlin, ambako uliwashwa. Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wanamichezo 3,000, nyota wa riadha Fritz Schilgen alipewa heshima ya kuubeba mwenge huo uwanjani
1964: Tokyo imekumbuka Hiroshima
Yoshinori Sakai-ambae anajulikana vilevile kama mtoto wa Hiroshima alizaliwa August 6,1945, siku ambayo Marekani iliangusha bomu la atomiki mjini Hiroshima. Alikuwa na umri wa miaka 19 tu pale alipobeba mwenge wa Olimpiki katika uwanja wa Tokyo, akionesha ishara ya amani ya ulimwengu na kukumbusha jambo lisilosahaulika katika kipindi cha Olimpiki.
1980: Kususia mashindano ya Moscow
Michezo ya Olimpiki haitengani na hali ya kisiasa. Dick Palmer, kiongozi wa timu ya Olimpiki ya Uingereza ameshika bango akiwakilisha chama cha Olimpiki cha taifa lake, akipinga Urusi kuivamia Afghanistan katika ufunguzi wa michezo hiyo mjini Moscow. Japan na Ujerumani Magharibi ni miongoni mwa mataifa yaliojiunga na Marekani kwa kutohudhuria michezo hiyo.
1996: Zama za kustaajabisha za Muhammad Ali
Mwenge ulipendeza ulipowashwa Barcelona, miaka minne baadae mjini Atlanta, ilikuwa furaha zaidi. Mwanamasumbwi Muhammadi Ali alikuwa mtu mwenye utata nchni Marekani baada ya kukataa kwenda kupigana vita vya Vietnam ingawa alikuwa shujaa ndondi na jitihada zake katika Uislamu. Wakati ukiwashwa mwenge 1996 alikuwa akitetemeka mikono kutokana na ugonjwa wa Parkinson.
2004: Vazi la dunia mjini Athens
Katika miaka ya hivi karibuni taratibu katika sanaa za maonesho katika hafla ya ufunguzi zimezidi kuwa muhimu zaidi ikilinganisha na awali, ingawa kauli mbiu ya amani imeendelea kubaki madhubuti. Mwaka 2004 mjini Athens ambako michezo hiyo ilizaliwa mwimbaji kutoka Iceland Bjork aliimba wimbo wake “Oceana” na alivaa ngua yenye kuonesha ramani ya dunia ya kubwa wa kilometa za mraba 10,000
2008: Mambo ya kustaajabisha mjini Beijing
Beijing ilitumua gharama kubwa katika hafla ya ugunguzi kwa kutumia dola milioni 100. Mwaka 2012 Uingereza ilitumia 2012. Kulikuwa na maonesho yasio na kifani ya ufunguzi yaliodumu kwa masaa matatu yalijumuisha washiriki 14,000.
2012: Kofia ya zamani kwa Malkia Elizabeth
Mjini London mwaka 2012, Malkia Elizabeth alikuwa mkuu wa kwanza wa taifa kufungua awamu mbili za michezo ya Olimpiki. Na alifanya hivyo kwa mitindo ambapo alitua kwa parachuti katika awamu ya kwanza ya michezo mjini Montreal 1976. Katika hotuba yake alitangaza rasmi kufunguliwa rasmi kwa Olimpiki 2012.