1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON:Utawala wa Myanmar waondoa amri ya kutotembea ovyo

20 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7E7

Utawala wa kijeshi wa Myanmar umeondoa amri ya kutotombea ovyo pamoja na kufanya mikutano amri iliyowekwa wiki kadhaa zilizopita wakati utawala huo ulipowavamia na kuwapiga watawa wakibudha walioanzisha maandamnao ya kuipinga serikali.

Utawala huo wa kijeshi aidha umetoa taarifa ya aina yake kupitia Televisheni ya serikali ya kutaka kufanya mazungumzo na kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi anayezuiliwa ndani ya nyumba.

Hatua ya Myanmar imekuja siku moja baada ya rais Gorge W Bush wa Marekani hapo jana kutangaza vikwazo zaidi dhidi ya viongozi wa utawala huo.Rais Bush aliamrisha kuongezwa kwa vikwazo vya sasa vya kibiashara,usafiri pamoja na kufungwa kwa akaunti za viongozi zaidi katika utawala huo wa kijeshi.

Aidha rais huyo wa Marekani aliusisitizia utawala wa Myanmar usiotaka Demokrasia uwaachie huru wafungwa wakisiasa na kuingia katika meza ya mazungumzo na chama cha Upinzani kinachotetea demokrasia.