Yajue mambo 10 kuhusu mji mkuu wa Ujermani
Berlin imekuwa kivutio cha watalii tangu kuanguka kwa ukuta wa Berlin mwaka wa 1989. Lakini ni watu wachache wanaotambua kwamba jiji hilo lenye tamaduni nyingi lina vitu vingi vya kuvutia sana.
Utamaduni ulioshamiri kupita kiasi katika sanaa ya opera (59625966)
Berlin ndio jiji pekee ulimwenguni ambalo lina jumla ya majumba matatu ya kumbi za utamaduni wa sanaa ya opera na kwa bahati nzuri sio ndoto vinginevyo zingekuwepo shughuli nyingi. Sababu ya kipekee ni kwamba kwa zaidi ya miaka 40, Berlin, kama nchi nzima, iligawanywa kati ya Mashariki na Magharibi, na ukuta wa Berlin uliosimama kwa miaka.
Ndoto ya mhandisi (48314306)
Ni rahisi kutoka eneo A kwenda eneo B mjini Berlin, kwani jiji hilo lina jumla ya madaraja karibu 2,100, zaidi ya 600 ambayo huvuka vyanzo halisi vya maji. Hii inashinda idadi ya madaraja huko Venice. Baada ya yote, kuna karibu kilomita 200 za mito na mifereji ambayo inaweza kupita boti, ikiwa ni pamoja na mto Spree, mto Havel na mfereji wa Teltow.
Fanya manunuzi mpaka vikudondoke! (43060482)
Mji ws Paris una maduka ya kifahari ya Lafayette, Madrid kuna El Corte Ingles, lakini Berlin inajivunia duka kubwa zaidi katika bara la Ulaya. Iilianzishwa mwaka wa 1907, Kaufhaus des Westens -Duka kubwa la nchi za Magharibi,duka linalofahamika Berlin kama KaDeWe,ni eneo lenye ukubwa sawa na viwanja vinane vya soka. Zaidi ya watu 50,000 huja hapa kununua kila siku, na asilimia 40 wakiwa watalii.
Mapishi ya kuzuzua
Wakati Rais wa Marekani wa wakati huo John F. Kennedy akitangaza "Ich bin ein Berliner"mimi ni mtu wa Berlin alimaanisha kitafunio maarufu Ujerumani kama Berliner, hata hivyo Berlin yenyewe, watu hutambua kama "Pfannkuchen" - ambayo ina maana ya chapati ya maji. Wakati chapati za maji halisi zinajulikana kama keki za mayai. Kuelewa lugha ya upishi huko Berlin inaweza kuwa changamoto sana.
Jiji lenye harakati(57952040)
Mojawapo ya maeneo bora zaidi mjini Berlin pa kufurahia bidhaa bora zaidi za kuoka na vyakula vingine maalum vya Kijerumani kwa kweli ni juu ya jengo la Reichstag! Huu ndio mkahawa pekee katika jengo la bunge duniani ambalo liko wazi kwa umma. Walakini, lazima ujiandikishe mapema, utoe maelezo ya kibinafsi na kuonyesha kitambulisho unapoingia kwenye jengo.
Vyakula vya tamaduni nyingi (53480317)
Ukizungumzia kuhusu chakula, jumuiya kubwa ya Kituruki ya Berlin ina ushawishi mkubwa juu ya vyakula vya ndani. Sasa unaweza kupata vyakula vya Kituruki katika maduka mingi ya mikate. Zaidi ya hayo, kuna maduka mengi ya Döner Kebab Berlin kuliko yaliyoko Istanbul! Sababu ni kwamba Kebab mtindo wake wa kipekee wa mikate ya sandwich na saladi na michuzi, ilivumbuliwa huko Berlin.
Hakuna nyama, tafadhali! (56244213)
Kwa wale ambao hawali nyama, kuna vyakula vingi mbadala huko Berlin. Jiji lina zaidi ya mikahawa 100 ya mboga mboga, inayoandaa vyakula na bidhaa zisizotokana na wanyama. maduka makubwa mengi, mikahawa na sehemu za aiskrimu pia hutoa bidhaa ambazo hazitengezwi na chochote cha wanyama. Kuna hata duka la bidhaa za ngono zisizotokana na bidhaa za wanyama.
Tuzungumze juu ya ngono! (19557588)
Ngono ina nafasi maalum huko Berlin. Hata kauli mbiu ya jiji isiyo rasmi inasema "arm aber sexy" (maskini lakini navutia) inaonyesha kipengele hiki cha utambulisho wa kisasa wa Berlin. Kwa watu wengi, ujinsia wao ni sehemu ya utamaduni wa jumla wa jiji. Kuna hata jumba la makumbusho la wapenzi wa jinsia moja na jumba la kumbukumbu la rangi za midomo linaloonesha mitizamo tofauti ya mapenzi.
Uzuri upo machoni mwa mtazamaji (37825535)
Ukiwa na maduka 300, Berlin ndio mahali pazuri zaidi barani Ulaya kwa sanaa ya kisasa. Iwapo uko sokoni kwa ajili ya sanaa fulani, Bila shaka Berlin ndio sehemu nzuri zaidi. Kuna makumbusho ya kiwango cha ulimwengu, ambayo mengi yao yameangaziwa karibu na Kisiwa cha Makumbusho. Berlin pia ni mwenyeji wa jumba kubwa la wazi la makumbusho ulimwenguni.
Hakuna haja ya kutazama ikiwa mvua itanyesha (59625755)
Hali ya hewa ya Berlin sio ya jua, lakini unajua kwamba kuna makumbusho mengi zaidi katika jiji kuu hilo kuliko idadi ya siku za mvua kila mwaka? Kwa hivyo, usiruhusu uvumi kuhusu hali mbaya ya hewa kukuzuia kuandaa safari yako inayofuata! Wasafiri mashuhuri watapanga safari zao kwa kuzingazia ukweli huu, wakitafuta maeneo mazuri katika siku za baridi wakati mvua haiachi kunyesha.