1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Xi, Modi waazimia kupunguza mivutano baina yao

25 Agosti 2023

Rais wa China Xi Jinping na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wamefanya mazungumzo ya "wazi na ya kina" kwa ajili ya kupunguza mivutano katika mpaka wao wenye unaozozaniwa na ambayo inaathiri uhusiano wao kwenye BRICS.

https://p.dw.com/p/4VZ66
BRICS-Gipfel in Südafrika
Picha: Themba Hadebe/AP/picture alliance

Haya yamesemwa na China hapo jana baada ya mkutano wa nadra wa ana kwa ana baina ya viongozi hao wawili.

Viongozi hao walikutana siku ya Alkhamis (Agosti 24) walipokuwa wakihudhuria mkutano wa kilele wa kundi la BRICS nchini Afrika Kusini.

Soma zaidi: Rais Xi aahidi kuisaidia Afrika kukuza viwanda vyake

Mahusiano kati ya nchi hizo mbili zenye idadi kubwa ya watu duniani hayajakuwa mazuri tangu kuzuka kwa mapigano katika mpaka wa Himalaya yaliyowauwa wanajeshi 20 wa India na wengine 4 wa China mwaka 2020.

Tangu wakati huo, makumi kwa maelfu ya wanajeshi wamepelekwa katika pande zote mbili za mpaka huo.

Wanajeshi hao wanasalia katika eneo hilo licha ya mizunguko 19 ya mazungumzo ya maafisa waandamizi wa jeshi kutoka nchi zote mbili.