1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Xi: China iko tayari kushirikiana na Ulaya

12 Januari 2024

Rais wa China Xi Jinping, amesema nchi yake iko tayari kuimarisha uhusiano wake na Ulaya. Matamshi hayo ameyatoa leo mjini Beijing katika mkutano wake na Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Alexander De Croo.

https://p.dw.com/p/4bBGc
Beijing, China | Rais wa China Xi Jinping akiwa na Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Alexander De Croo.
Rais wa China Xi Jinping akiwa na Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Alexander De Croo. Picha: Huang Jingwen/Xinhua/picture alliance

De Croo aliwasili jana China, kuhudhuria ufunguzi wa ubalozi mpya wa Ubelgiji mjini Beijing na kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi. 

Soma pia:China yaunga mkono Somalia kulinda mamlaka na mipaka yake

Xi amemwambia De Croo kuwa China iko tayari kufanya kazi na Umoja wa Ulaya ili kukuza maendeleo thabiti katika uhusiano wa China na umoja huo.

China na Umoja wa Ulaya ni washirika wakubwa wa kibiashara, lakini umoja huo hivi karibuni umeonyesha nia ya kupunguza utegemezi kwa China katika teknolojia na maeneo mengine. De Croo pia amekutana na Waziri Mkuu wa China, Li Qiang.