Xi, Biden wapongezana kuadhimisha miaka 45 ya kidiplomasia
1 Januari 2024Katika ujumbe wake, Xi amesema kuwa nchi zote mbili "zimestahimili misukosuko na kusonga mbele kwa ujumla", hali ambayo imeboresha ustawi wa watu wao na kuchangia amani ya ulimwengu, utulivu na ustawi.
Xi ameongeza kuwa yuko tayari kushirikiana na Rais Biden kuendelea kuimarisha uhusiano wa mataifa hayo mawili kwa manufaa ya raia wao na kuendeleza amani na maendeleo ya dunia.
Soma pia: Xi na Biden wawasili San Francisco kwa mazungumzo muhimu
Mahusiano Mkutano wa marais wa Marekani na China una maana gani kwa Ujerumanikati ya China na Marekani yamekuwa magumu lakini maafisa wa utawala wa Biden wamefanya ziara nchini China na kukutana na wenzao kujenga upya mawasiliano na uaminifu katika miezi iliyotangulia mkutano wa kilele kati ya Xi na Biden huko San Francisco mnamo mwezi Novemba, ulioonekana kuwa fursa ya kupunguza mvutano kati ya nchi hizo mbili zenye uchumi mkubwa duniani.