XI, Biden kukutana chini ya kivuli cha kurejea kwa Trump
16 Novemba 2024Mkutano huu unalenga kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na China huku ukilenga pia kuhakikisha ushindani haugeuki kuwa mgogoro. Trump ameashiria msimamo mkali dhidi ya China, akitishia ushuru wa asilimia 60 kwa bidhaa za China.
Biden na Xi wameonya kuhusu nyakati za misukosuko zijazo, huku Biden akisisitiza umuhimu wa ushirika wake na Japan na Korea Kusini. Trump amerudi na sera ya "Amerika Kwanza" ambayo inaweza kuhatarisha ushirikiano uliopo kwenye masuala ya kimataifa.
Soma pia: APEC kuzingatia zaidi masuala ya usawa na mazingira
Jumuiya ya APEC, iliyoundwa mwaka wa 1989 kwa lengo la kukuza biashara huria ya kikanda, inazijumuisha nchi 21 ambazo kwa pamoja uchumi wake unawakilisha takriban asilimia 60 ya pato la taifa la dunia na zaidi ya asilimia 40 ya biashara ya kimataifa.