1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WTO kuongozwa na mchumi kutoka Afrika

15 Februari 2021

Shirika la Biashara Ulimwenguni, WTO linatarajiwa kwa mara ya kwanza kuongozwa na mtu kutoka barani Afrika kuanzia Jumatatu.

https://p.dw.com/p/3pMyR
Ngozi Okonjo-Iweala | nigerianische Politikerin
Picha: Martial Trezzini/KEYSTONE/picture alliance

Mchumi mwandamizi kutoka Nigeria Ngozi Okonjo-Iweala, ambaye pia ni mwanamke wa kwanza kuchukua wadhifa huo, ndiye mgombea pekee aliyesalia katika shirika hilo lenye makao yake mjini Geneva.

Hata hivyo, uteuzi wake kama mkurugenzi mkuu katika mkutano wa wajumbe kutoka kwa nchi wanachama 164 wa WTO unachukuliwa kama utaratibu tu na wala usioaminika kwa dhati.

Utawala wa aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump ulikuwa ulipinga uteuzi wake japo Rais wa sasa Joe Biden amemuunga mkono Okonjo-Iweala ambaye aliwahi kuhudumu kama waziri wa fedha na waziri wa mambo ya nje wa Nigeria, pamoja na kuhudumu kama mkurugeni mkuu wa Benki ya Dunia.

Soma zaidi: Marekani yatatiza juhudi za WHO za kupata kiongozi

Okonjo-Iweala aliwashinda wagombea wengine kadha katika kinyang'anyiro hicho akiwemo mpinzani wake mkuu, Waziri wa Biashara wa Korea Kusini, Yoo Myung Hee.

 

(DPA)