Wolfsburg. VW yathibitisha kuwafuta kati maelfu ya wafanyakazi.
6 Septemba 2005Kampuni kubwa kabisa linalounda magari barani Ulaya Volkswagen, limethibitisha mipango ya ya kupunguza maelfu ya wafanyakazi nchini Ujerumani.
VW imesema kuwa inahitaji kupunguza ziada ya wafanyakazi wake ghali wa Ujerumani ili kuweza kupata faida.
Lakini , mwenyekiti mtendaji wa kampuni hilo Bernd Pitschetsrieder amesema kuwa anataka kuepusha hali ya kuwafuta kazi na badala yake kuwapa vivutio wafanyakazi hao ili kuondoka kwa hiari yao.
Inafikiriwa kuwa kiasi cha wafanyakazi 10 ,000 , wengi wao wakiwa wanakaribia umri wa kustaafu wanaweza kufanya hivyo mapema , na watapatiwa vivutio kadha. Volkswagen hivi sasa inaajiri kiasi cha wafanyakazi 103,000 katika viwanda vyake sita nchini Ujerumani.