WISMAR: Vijana wajadili mabadiliko ya hali ya hewa
3 Juni 2007Matangazo
Kabla ya kufunguliwa mkutano wa kilele wa G-8, mjini Heiligendamm nchini Ujerumani,vijana pia kutoka sehemu zote za dunia wamekusanyika kaskazini mwa Ujerumani katika mji wa Wismar. Vijana hao wanahudhuria mkutano wa kilele wa vijana-Junior 8.Zaidi ya vijana 70 wanajadiliana juu ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani,uchumi wa bara Afrika na ulinzi wa hakimiliki.Mkutano huo wa vijana ulifunguliwa na waziri wa maendeleo wa Ujerumani Bibi Wieczorek-Zeul.