WINDHOEK: Balozi wa Ujerumani nchini Namibia, Wolfgang Massing, amesikitika ...
12 Januari 2004Matangazo
kwa niaba ya serikali ya Ujerumani, jinsi uasi wa Waharero ulivyokandamizwa kikatili na ukoloni wa kijerumani miaka 100 iliopita. Wakati wa mapigano ya wakati ule katika koloni hilo la zamani la kijerumani, kuanzia mwaka 1904 hadi 1907, kiasi Waharero 60 elfu waliuawa. Lakini Ujerumani inakataa kutaka radhi rasmi na kadhalika ulipaji fidia. Balozi Massing alitoa sababu kuwa msaada wa Ujerumani haupendelei kabila fulani. Ujerumani ni mfadhili wa safu ya mbele wa Namibia, na tangu mwaka 1990 imeipa msaada wa maendeleo wa EURO Millioni 500.