WIESBADEN: Mradi wa kujikinga uendelezwe chini ya mfumo wa NATO
3 Machi 2007Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung amesema,mradi wa Marekani kuhusu utaratibu wa kujikinga dhidi ya makombora,unapaswa kuendelezwa chini ya mfumo wa shirika la kujihami la magharibi NATO.Baada ya mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya mjini Wiesbaden,Jung alisema,shaka za Urussi kuhusu utaratibu huo uliozusha mabishano,zinaweza kuondoshwa kwa kufanywa majadiliano kati ya NATO na Urussi. Marekani,inapanga kuwa na mfumo huo wa kujikinga dhidi ya makombora yenye masafa nchini Poland. Rais Vladimir Putin wa Urussi hivi karibuni katika mkutano wa usalama uliofanywa mjini Munich,kusini mwa Ujerumani alisema,hakuna haja ya kuwa na mradi wa aina hiyo.Wakati huo huo akaionya NATO dhidi ya kuongeza miundo yake katika Ulaya ya Mashariki.